|
||||
Moshi Diocese at P.O. Box 3011, Moshi, Kilimanjaro n/a TZ - Mwondoko wa Awamu Mpya - MH. ASKOFU AMANI
Kwa vile jimbo letu limeshaadhimisha miaka 100 ya imani, tunamshukuru Mungu kwa urithi wa Injili na maendeleo yote waliotuletea Wamisionari. Wazee wetu walipokea imani, wakaifanyia kazi na sasa ni zamu yetu tuiendeleze na tukolee zaidi katika tamaduni za kikristo. Ulimwengu wa leo unahitaji ushuhuda wa dhati kutoka kwetu sisi tunaotegemewa kuwa chumvi na mwanga katika sekta zote za maisha. Utambulisho wetu hasa ni kuwa chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu. Je! Uwepo wetu katika jamii huleta matumaini kwa watu na utukufu kwa Mungu? (Mt. 5:13-16).Kweli ukristo ni changamoto kubwa. Tutumie tuliyo nayo hasa taasisi zetu Sisi sote tumkiri Kristo kuwa Bwana na Mkombozi wetu na kuachana na desturi za kutafuta usalama kwa mizimu, waganga wa ramli na wapiga bao yaani fikra na matendo ya kishirikina. Hali kadhalika, fikra za kibaguzi na dharau kati ya watumishi wa Mungu sio za kimungu bali za yule mwovu kwa uhakika. Mila, tamaa, desturi na mazoea yanayopingana na maagano ya ubatizo ni fedheha tupu kwa mfuasi wa Yesu.. Ibilisi akiotesha ndago hutumia vibarua wake kuzipalizi. Mtume Pauli anatuasa: “Basi, acheni mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa tamaa zake danganyifu. Jirekebisheni upya rohoni na katika fikra zenu. Vaeni hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionesha katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu” Ef.4: 22-24. Basi, sisi sote twatakiwa tuishi maisha ya shukrani kwa kushika amri za Mungu na kushika kiaminifu viapo vyetu vya Ubatizo, Komunyo ya kwanza, Kipaimara, Ndoa, Nadhiri na Daraja. Hiyo ndiyo njia itakayotuwezesha kupokea mwanga wa Kristo na jimbo letu litakuwa na baraka za miito yote kwa wingi. Hayo ndiyo matumaini yangu wakati tunapoanza awamu ya kipindi kipya jimboni. Kwa njia ya kuwajibika na kushirikiana katika Kristo tutafikia umoja tulioombewa na Kristo kwenye sala yake maalum kwa wafuasi wa nyakati zote.(Yoh. 17). Kwa sasa, wafuasi ni sisi, wewe na mimi; kila mwamini katika kazi na nafasi yake kwenye jamii. Tuombe mwanga wa Roho Mtakatifu wa kuona na kuoneshana njia itupasayo kupita, na ujasiri wa kushirikiana katika kuyakabili matatizo na pingamizi za maisha kwa matumaini tukiyazingatia maneno ya mtume Paulo kuhusu upendo wa Mungu kwetu: “Tumepata ushindi mkubwa kwa msaada wake yeye aliyetupenda. Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu” Rom.8:37b-39. NEMBO Sikukuu ya Ukulu wa Mt. Petro Mtume hufanyika tarehe 22 Februari. Sikukuu hii imeadhimishwa Roma tangu karne ya nne. Hii ni alama ya umoja wa Kanisa lililojengwa na Kristo juu ya mwamba mtume Petro. Mt.16: 18 – 19. Ni siku maalum ya kuomba mshikamano na ustawi wa Kanisa jimboni na ulimwenguni kote. Maklero, watawa na walei kwa pamoja washirikiane kutekeleza majukumu yawapasayo Nimeichagua tarehe hii iwe siku ya kuwekwa kwangu wakfu kwa sababu hitaji letu kubwa hapa Jimboni Moshi ni mshikamano utakaotokana na kuwajibika na kushirikiana katika Kristo. Kanisa haliwezi kuwa hai na la mafanikio wanakanisa wasipowajibika na kuchangia nguvu kwa pamoja. Ninaamini tunaweza kufikia malengo ya kiinjili endapo tutayafanyia kazi kwa pamoja. Baada ya uteuzi kutangazwa, askofu mteule aliambiwa aandae NEMBO. Nembo hukusudiwa ioneshe TASWIRA ya uchungaji. Kaulimbiu ninayoweka mbele yangu ni: “KUWAJIBIKA NA KUSHIRIKIANA KATIKA KRISTO”. Tunapoanza awamu mpya ya Jimbo letu, natafakari jimbo ambalo limeshaadhimisha miaka 100 ya kupokea imani ya kikristo. Tumefikia hatua ya kufurahia matunda ya miaka karibu 120 ya imani na kuimarisha tuliyo nayo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Namna yetu ya kuishi imani kiinjili inatuwajibisha tumtazame na tujiunge kwa umakini zaidi na Mkombozi wetu. Yeye ametuita kutoka gizani na kutuweka katika mwanga wa maisha mapya ya neema. Mtume Petro anaeleza vizuri anaposema: “Kwa uwezo wake wa kimungu, Mungu ametujalia mambo yote tunayohitaji ili tuishi maisha ya kumcha Mungu kwa kumjua yeye aliyetuita tuushiriki utukufu na wema wake yeye mwenyewe.” 2Pet. 1:3. TULIKOTOKA Wamisionari watatu wa Shirika la Roho Mtakatifu walifika Kilimanjaro kwa mara ya kwanza tarehe 15 Agosti 1890 wakiongozwa na Askofu wa Vikarieti ya Zanzibari Mhashamu Jean Marie Raoul de Courmont. Wengine walikuwa mapadre Auguste Commenginger na Alexander Le Roy pamoja na wapagazi Nderingo na wenzake wachache. Ujio huo ulifungua Kilimanjaro kwa utume wa kijasiri wa wamisionari kwa muda wa miaka 20. Juhudi kubwa za kusimika Injili katika eneo hili zilizaa matunda pale Papa Pius X alipoafiki ombi la kuwepo kwa Vikarieti ya Kilimanjaro. Alimteua Askofu Maria Joseph Aloyse Munsch kuwa mtawala wake kuanzia tarehe 13 Septemba 1910. Eneo husika ni majimbo tunayofahamu leo kuwa Tanga, Same, Moshi, Arusha, Mbulu na sehemu ya jimbo la Askofu Henry Aloyse Gogarty alisimamia Vikarieti 1922-1924 na kuwa Mtawala wake 1924-1931. Mhashamu Gogarty aliona umuhimu wa kuandaa Wainjilishaji wazawa ili wapeleke Injili mbele. Kauli mbiu yake ilikuwa: “O ORIENS VENI ET ILLUMINA” (NYOTA YA MASHARIKI NJOO UANGAZE). Aliamini kwamba Elimu na malezi vingeleta mwanga katika maisha ya Kanisa changa. Alifungua seminari ya Mt. Yakobo Kilema Chini mwaka 1925 kwa ajili ya kuandaa mapadre wa vikarieti ya Kilimanjaro na hata Askofu Joseph Byrne alitawala Vikarieti Kilimanjaro (1933-19530 na Jimbo Moshi (1953-1959). Kauli mbiu yake ilikuwa: “SUB TUUM PRAESIDIUM” (TUNAUKIMBILIA ULINZI WAKO). Alikuwa na heshima kubwa Mbulu ilikabidhiwa kwa Wapalotini ( Tanga ilifanywa ‘Prefecture’ na kukabidhiwa kwa Shirika la Rosminiani( Moshi ilifanywa kuwa Jimbo tarehe Awamu ya pili ilimwangukia Padre mzawa na pia mtawa wa Shirika la Roho Mtakatifu aliyepewa uaskofu na Papa Yohani XXIII tarehe Awamu ya tatu: Monsinyori Joseph A. Sipendi aliyekuwa mtawala wa jimbo la Kipapa Aliona Kanisa linao wajibu wa kuwasaidia watu waishi kama binadamu katika kupata mahitaji Awamu ya nne: Kwa takribani kipindi cha mwaka moja, jimbo liliongozwa na Mtawala Jimbo Msgr. Arbogast Sekundo. Awamu hii ilimwangukia aliyekuwa Padre Mlesi wa miito jimboni, Mhashamu Amedeus P. Msarikie. Alipewa daraja la Uaskofu tarehe Askofu Msarikie aliieleza azma yake katika kaulimbiu:UMOJA KATIKA UPENDO, yaani mshikamano wa kijimbo. Alihimiza uimarishaji wa uchungaji kwa kuboresha malezi ya waseminaristi, watawa na mapadre. Aliendeleza uboreshaji wa huduma za afya na elimu jimboni pote. Alihimiza ujenzi bora wa makanisa, nyumba za mapadre, konventi za watawa na utunzaji wa mazingira. Aliimarisha ofisi kuu ya Jimbo na idara zake kwa ajili ya kuboresha huduma za kichungaji hapa jimboni na hata kushiriki ngazi za kanda na kitaifa. Shirika la Mabradha wa Jimbo lilifanyiwa marekebisho na kupewa jina Mabradha wa Yesu Mkombozi na makao Kwa kuzingatia alama za nyakati hususan kuboresha elimu, Askofu Msarikie ameanzisha Chuo Kikuu cha Mwenge MWUCE kwa lengo la kuandaa walimu bora wa kufundisha shule za Sekondari za jimbo na Seminari. Amejenga kituo cha Moyo Mt. wa Yesu Longuo kwa ajili ya kuwa na nyumbani kwa mapadre na kituo cha malezi endelevu. Amejenga kituo cha ufundi Karanga kuwasaidia vijana kujiandaa kwa utumishi wa jamii. Askofu Msarikie alifanikisha mengi jimboni na taifani. Wakati wa awamu yake alikazana kuimarisha umoja na mshikamano wa kijimbo pia alihimiza ufundishaji dini shuleni na vyuoni. Mara nyingi alihimiza uchungaji sahihi na makini Mhashamu alisimamia vyema matayarisho na maadhimisho ya Yubilei ya miaka 100 ya Ukatoliki Moshi na kumkaribisha hayati Papa Yohane Paulo II hapa Moshi Septemba 4-5,1990. Alihimiza pia matayarisho na adhimisho la Yubilei ya Ukombozi mwaka 2000 iliyofanywa kiulimwengu. Ama kweli awamu hii ilikuwa na matukio makubwa ya kusherehekea. Mwaka 2003 Jimbo liliadhimisha Yubilei ya Dhahabu (miaka50). Tunapotafakari mwaka huu wa JNNK tunazidi kutiwa moyo na msisitizo wa Askofu Msarikie wa malezi endelevu ya Halmashauri Walei na vyama na mashirika ya kitume ili watu wote wa Mungu wazidi kukomaa katika kumjua Mungu na kumpenda yeye na jirani. Askofu Msarikie ametumia muda na nguvu zake nyingi na sadaka mbalimbali katika utume wake jimboni na taifani. Amekuwa mkarimu kwa kushirikisha vipaji vyake akaliongoza na kuliendeleza jimbo la Moshi kwa miaka 21 mpaka alipostaafu akiwa na afya na nguvu tele na kukabidhi jimbo kwa askofu wa awamu ya tano, ndiyo awamu mpya inayoelezwa hapa. Tunapotafakari historia ya jimbo letu tujione katika mpango Mwenyezi Mungu aliofichua kwetu. Kwanza ni kumshukuru Mungu kwa makuu aliyotutendea Tunapenda basi nembo husika ioneshe ni kwa namna gani tutapokea Injili, kuifanyia kazi na kufurahia matunda yake. Paulo mtume anatuuliza Wamoshi: “Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, mapendo yake yanawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana ninyi kwa ninyi? Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikra moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja.” Fil. 2: 1-3. Jibu letu liweje? Tupitie alama katika nembo: Nembo itakuwa na alama 7: Msalaba, Biblia, Ekaristi, Nyota, Mlima Kilimanjaro, Tambarare ya kijani na Kauli mbiu yenyewe. 1.Msalaba: Tumekombolewa kwa upendo wa ajabu kwa njia ya msalaba wa Mkombozi wetu na twatakiwa tufahamike kuwa wafuasi hai : “ 2.Biblia: Mungu husema nasi kwa njia ya Maandiko Matakatifu. Yesu anatuambia: “ 3.Ekaristi:”Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaa ndani yake”Yoh. 6:56. Hatuna njia bora ya kushikamana na Mungu wetu kuliko kuungana na Mwanaye katika sakramenti ya Ekaristi. Huu ni mkate hai ulio tofauti na lishe nyingine zote. Yesu mwenyewe anasema: “Mimi ni mkate hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akila mkate huu ataishi milele. Na mkate nitakaompa ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili ya uhai wa ulimwengu” Yoh. 6:51. Kwenye nembo Ekaristi imezungukwa na rangi ya zambarao kuonesha kwamba yatupasa tujitakase kwa toba kabla ya kushiriki meza ya Bwana tusije tukajiingiza hukumuni kwa njia ya mwili na damu ya Bwana 1Kor.11:27. Tena “Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu 4.Nyota: Nyota iliwaongoza Mamajusi mpaka mahali alipozaliwa Mwokozi. Mwokozi wetu anatuambia: “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uhai.Yoh. 8:12. Tuwe na imani thabiti na Mkombozi wetu. Hakuna mwingine wa kutegemewa isipokuwa huyo aliyetimiza kikamilifu mpango wa Baba wa kutufanya huru: “Nami nitakapoinuliwa juu ya nchi nitamvuta kila mmoja kwangu” Yoh. 5.Mlima Kilimanjaro: Kibo na Mawenzi: Hili ndilo jimbo letu. Mungu mwenyezi ametupa mahali bora na pazuri pa kuishi. Watu wengi duniani wanatamani wangeishi mahali hapa. Makundi kwa makundi huja kutalii na kushuhudia utukufu wa Mungu ulio katika hifadhi ya Kilimanjaro.”Mungu alipoumba kazi zake mwanzoni, alizifanya ziwepo na kuzipa mpango, akazipa mpango wa kufuata milele, tangu mwanzo wake na vizazi vyote” Sira Yatupasa kutunza mazingira tuliyopewa na Mungu yakiwa ni urithi wa hapa duniani. Njia bora ya kuthamini urithi ni kuuheshimu, kuutunza na kuuendeleza. Tunapotazama Kibo na Mawenzi tukumbuke fadhili zote za Mungu na tuhimizane kuboresha mazingira tunamoishi. Kwa mantiki hiyo hiyo tukazane kulitunza na kuliendeleza Kanisa jimboni, taifani na ulimwenguni. Tujenge tabia ya kuthamini na kutunza yaliyopo, na kuyaendeleza kwa kuboresha huduma na maisha. Ni heshima na fahari kutunza mazingira; ni aibu na fedheha kuharibu au kutelekeza urithi tuliopewa na Mungu na vizazi vilivyopita. Tutaachia kizazi kijacho urithi gani? 6.Tambarare ya kijani. Hawa ndio wakazi wa Kilimanjaro hasa wa jimbo la Moshi. Watu wote wanaoishi katika eneo hili ndio utajiri wa kwanza wa taifa na kanisa. Kanisa la Moshi kimsingi lina makundi matatu: Walei, Watawa na Maklero. Kila kundi lina umuhimu na umaarufu wake katika uhai wa Kanisa. Mtaguso wa pili wa Vatikano uliainisha vizuri jinsi makundi hayo yanavyopaswa kushirikiana na kutajirishana kwa lengo la kuishi Injili kwa umakini kwani changamoto za ulimwengu wa leo zadai hivyo. Rangi ya kijani yaashiria hali ya kuchipua na kusitawi kwa waamini wa ngazi zote. Hiyo ni changamoto ya kumkaribisha Roho Mtakatifu atuwezeshe kushika nafasi zetu katika mpango wa Mungu ambao ni “kukusanya pamoja viumbe vyote, kila kitu mbinguni na duniani, chini ya Kristo” Ef. MAISHA HALISI. a). Mklero anatarajiwa kuwajibika na kushirikiana na watu mbalimbali ili mpangilio wa matumizi ya muda na nguvu zake udhihirishe kwamba aliwekwa wakfu kwa ajili ya kushiriki ukuhani wa Kristo mwenyewe. “Kila kuhani mkuu ambaye huchaguliwa miongoni mwa watu hupewa jukumu la kushughulikia mambo ya Mungu kwa niaba ya watu, kutolea zawadi na dhabihu kwa ajili ya dhambi” Ebr. 5:1. Mklero anategemewa na Mungu, Mama Kanisa, waamini na watu wote, awajibike na yale yote aliyoahidi kama alivyotamka alipopewa daraja la Upadre. Kwamba alitoka kwenye familia tajiri au maskini, wasomi au wasio wasomi, katoka kaskazini au mashariki, ukoo huu au ule: yote hayo yanasawazishwa na wito wa kufanya kazi katika shamba la Bwana kwa ushirikiano na wafanyakazi wenzake. Tangu mwanzo Yesu aliwateua “watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri na wawe na uwezo wa kuwafukuza pepo” Mk. b). Mtawa anategemewa atoe ushuhuda wazi kwamba hakugawanyika bali “hujishughulisha na mambo ya Bwana apate kujitolea mwili na roho kwa Bwana” 1Kor.7:34a. Maisha ya mtawa yatoe unabii kwamba mwanadamu asivurugike akili akihangaika juu ya chakula na chakunywa bali Injili yamdai awekeze katika Ufalme sasa na mengine yote atapewa kwa ziada. (Lk.12: 29-31). Ulimwengu unahitaji kuona mifano ya wanaume na wanawake walio na furaha na hali ya kutosheka kwa kumchagua Bwana awe urithi wao. Basi mtawa atoe ushuhuda wa kuishi Injili kwa kufuatana na viapo vya nadhiri au ahadi zake kwa Mungu, kwa Kanisa na kwa Shirika. Taifa la Mungu linahitaji watawa wanaojitoa kwa sala, kwa sadaka na kwa kutoa huduma za kuleta mapinduzi ya kiinjili katika maisha ya watu. Vijana na watoto waone ushujaa katika maisha na utume wa watawa. Mtindo wa maisha c). Mlei ana nafasi na wajibu wa kipekee wa kufikisha mwanga wa Injili katika sekta zote za maisha ya mwanadamu kwa vile anafika kote huko. Kwa mujibu wa Ubatizo na Kipaimara mwamini Mlei anaambiwa yeye kuwa ni chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu. Wajibu wake DIRA YETU. 7.KAULI MBIU: Kutokana na maelezo ya hizo alama kwenye nembo, maneno yatakayoeleza azma ya awamu hii ni: KUWAJIBIKA NA KUSHIRIKIANA KATIKA KRISTO. Mtume Paulo anaeleza uhai wetu wa imani akitumia mfano wa mwili mmoja ulio katika ushirikiano wa viungo vingi. “Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili Yesu mwenyewe anahimiza kuwajibika NAMNA BORA YA KULEA IMANI NI KUWA NA MSIMAMO MMOJA JIMBONI. TARATIBU ZA HUDUMA ZA SAKRAMENTI JIMBONI MOSHI. “Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na kuishiriki hali yake ya kimungu” 2Pet.1:4. I. UBATIZO: 1. WATOTO WACHANGA i. Mara mtoto azaliwapo fomu ichukuliwe ofisini ikajazwe jumuiyani. ii. Baada ya kujazwa vizuri katika JNNK fomu ipelekwe kwa Padri mlezi kwa maelekezo muhimu juu ya semina na ubatizo. Kila JNNK iwe na muhuri na utumike kuidhinisha mambo ya JNNK. iii. Wazazi na msimamizi wa ubatizo wahudhurie semina ya uwajibikaji na ushuhuda wa imani kwa siku moja kabla ya ubatizo. Kubatiza ni kumzaa mtoto kiroho! iv. Ubatizo wa wachanga ufanyike siku mwafaka ambayo wazazi wote wawili ( 2. WATU WAZIMA. i. Wajiandikishe ofisini kwa ajili ya mafundisho ya dini na Biblia. ii. Wahudhurie mafundisho mpaka wayajue na kushinda mitihani pamoja na kulipa ada. iii. Wajaze fomu za kuomba ubatizo kupitia JNNK zao na kuzipeleka fomu kwa Padri kiongozi wa mafundisho ya dini. iv. Watu wazima hupata Sakramenti za awali yaani Ubatizo, Kipaimara na Ekaristi, zote kwa wakati mmoja. v. Wakristo wasio wakatoliki hupewa mafundisho ya katekisimu na kupokelewa rasmi kwenye ukatoliki kwa ibada maalum. Kushirikiana na wakatoliki kwenye ibada na JNNK haitoshi kumwingiza mtu kwenye imani Katoliki! Jambo hili lisifanywe kwa kulipua na haraka. II. EKARISTI TAKATIFU AU KOMUNYO YA 1. WANAFUNZI – SHULE YA MSINGI. i. Wanafunzi wa darasa IV na la V wenye kufahamu sala waandikishwe katika JNNK kwa kulipa ada itakayotumika kuwaandalia mitihani ya kuandika. Watafundishwa kwa mwaka mmoja na kila mmoja awe na katekisimu ya mafundisho. ii. Wahudhurie mafundisho kiaminifu na washinde mitihani kwa kupata alama 50-100. Padri asimamie kwa makini zoezi lote la maandalizi. iii. Waboreshe tabia zao ziendane na mafundisho waliyopewa. Wazazi na wasimamizi wa ubatizo pamoja na viongozi wa JNNK wasimamie malezi kwa ushirikiano. iv. Walioshinda mitihani waungame vizuri na walipe ada v. Wanafunzi watapokea Komunyo ya kwanza tarehe watakayopangiwa na Paroko. III KIPAIMARA: WANAFUNZI – SHULE YA MSINGI. i. Wanafunzi darasa la V na la VI waliokwishapokea Ekaristi waandikishwe katika JNNK kwa kulipa ada kwa ajili ya mitihani. Wataffundishwa kwa mwaka mmoja na kila mmoja awe na Katekisimu ya Biblia na Biblia (Ziko Bookshop). ii. Wahudhurie mafundisho kiaminifu, wakomae kitabia na washinde mitihani kwa Kupata alama 50-100. Padri na mkatekista mhusika wasimamie maandalizi yote iii. Mafundisho yawawezeshe kukomaa kimaadili, yawape kionjo cha imani ya matendo ya kweli. iv. Walioshinda mtihani waungame vizuri na kulipa ada watakavyoelekezwa. v. Wanafunzi watapokea Kipaimara tarehe watakayopangiwa na Paroko. vi. Wasimamizi wa Ubatizo wasishinikizwe kugharamia sherehe za maadhimisho. 2. WANAFUNZI -- SEKONDARI NA VYUO: i. Wanafunzi waanze mafundisho ya Katekisimu mara wafunguapo shule. Wajizoeshe Biblia na kuhamasishwa kuwa na KKK ufupisho makini. ii. Majina ya hao wanaoandaliwa mashuleni yafikishwe ofisini na vyeti vyao vya ubatizo viwe tayari kwa mwalimu mlezi mwezi Juni. iii. Watafanya mtihani mwanzo wa mwezi Septemba na watalipia mtihani huo. Padri mlezi wa parokiani ahusike na utaratibu huu. iv. Watakaoshinda watalipa ada ya sakramenti na kuwasilisha vyeti vya Ubatizo. v. Wanafunzi wa Sekondari na Vyuo watapokea Kipaimara Septemba baada ya kupokea sakramenti ya Kitubio(wachache hupokea Ubatizo na Ekaristi siku chache kabla ya Kipaimara kutegemea na maandalizi waliyopewa). IV SAKRAMENTI YA KITUBIO (UPATANISHO). i. Kila mkristo apokee Sakramenti hii ili awe katika hali ya neema. ii. Maungamo yapangiwe utaratibu unaoeleweka kwa waamini na ufuatwe. V. SAKRAMENTI YA NDOA. i. Wachumba wakiwa na vyeti vya ubatizo wasindikizwe ofisini na kiongozi JNNK ili wakaandikishe ndoa. Wawe na kibali cha wazazi wa pande zote mbili. ii. Wakati ndoa ikitangazwa, mafundisho ya Kanisa juu ya sakramenti ndoa na majukumu yake yatolewe kwa dhati, kwa muda wa kutosha na kwa siku maalum. iii. Yafaa wachumba wapate vitabu vya kuimarisha imani na mahusiano iv. Ndoa yaweza kufungwa wakati wa kufaa maarusi wakisha maliza mafundisho v. Maarusi na wapambe wavae mavazi ya heshima na ya kiibada, tena wawepo kiroho katika ibada wakiombea udumifu na usitawi wa ndoa hiyo. VI. SAKRAMENTI YA WAGONJWA. i Mwanafamilia apelike taarifa kwa kiongozi JNNK kuhusu hali ya mgonjwa na sakramenti anayohitaji. ii. Kiongozi JNNK amwendee Padri mlezi kuhusu hitaji la mgonjwa ili taratibu za huduma zipangwe. iii. Padri mlezi anaweza kupanga na uongozi JNNK Mtaa/ Kanda namna ya kuwafikia wagonjwa muda wowote lakini hasa wakati wa Pasaka. iv. Wagonjwa wasicheleweshwe kupelekwa hospitali. v. Meza yenye kitambaa VII: WANAOPENDA KUWA MAPADRE NA WATAWA: i. Mwenye kusikia msukumo wa kuwa Padri au Bradha au Sista amwone Padri mlezi wa JNNK ili aelekezwe taratibu za kufuatilia wito wake. Inafaa watoto na vijana wajiunge na Mashirika ya Utoto wa Yesu, Lejio, Bikira Maria, ii. Baba na Mama familia wawe makini kuilea miito ya Mungu na Kanisa katika mazingira ya upendo wa kiristo yaani sala, kuthaminiana na ushirikiano ndani ya familia VIII MAZIKO. i. Kifo cha mkristo kikitokea ripoti ifikishwe mapema kwa Padri mlezi wa JNNK. Daftari ya mahudhurio jumuiyani ipelekwe ofisini ili iwasaidie Padri mlezi, Kiongozi JNNK na Mwanafamilia kupanga taratibu za maziko. ii. Endapo Padri hataweza kuadhimisha ibada ya maziko, amwandae Mhudumu Mlei (Mkatekista) kutoa huduma hiyo. iii. Ikiwa mkristo amefariki nje ya eneo anamoishi na kufahamika, barua ya Padre aliyemhudumia kiroho itahitajika kueleza iv. Ikumbukwe kwamba maziko ya kikristo ni heshima apewayo mkristo aliyeishi imani pamoja na waamini wenzake. Maziko sio Sakramenti. HITIMISHO. Kazi kubwa kwetu sasa ni kupata MALEZI YA FIKRA, DHAMIRA NA MOYO ILI TUWEZE KUTEMBEA PAMOJA. Twahitaji Semina za stadi za maisha ya kijamii na ya kiroho, mafungo, warsha, maigizo na hasa kupanga malezi endelevu kwa vikundi mbalimbali Pamoja na malezi, tunapaswa kuchukua hatua za makusudi tuwe na mawasiliano sahihi na ya ukaribu zaidi. Watu wanaoishi pamoja wazungumze na kupanga mambo kwa pamoja. Viongozi bora hushirikisha wanaoongozwa ili nao washirikishe mawazo KARIBU BASI TUWAJIBIKE NA TUSHIRIKIANE KATIKA KRISTO. Imetolewa Sikukuu ya Pentekoste Mei 11, 2008 + Isaac Amani. Askofu Jimbo Moshi. Haki zote zimehifadhiwa. |
||||
|
P.O Box 3041 Moshi, Tanzania. Tel. +255-27-2752157 [Chancery], +255-27-2752089 Fax: 0255-27-2750934.[Bishop's House] Web. www.moshidioces.org Email; bishopshouse_moshi@yahoo.co.uk This site is hosted by CatholicWeb.com | TheCatholicDirectory.com Powered by CompBiz EZWeb© software. Server management powered by Spiderhost. |
||||